Friday 17 July 2015

Shujaa Wa Kwetu



eduuuu.jpg

Given Edward ni Kijana wa kitanzania mwenye miaka ishirini. Kijana huyu wa kitanzania ni shujaa wangu na kijana ambaye amehamisisha si tu vijana bali watu wa rika mbali mbali. Given amekulia katika maisha ya shida sana; ambapo wakati anasoma shule ya msingi ilimbidi kuamka asubuhi sana ili kuweza kufika shuleni kwa wakati.
Kwa nini Given ni shujaa kwangu? Mwaka 2014 mwezi wa pili Given alianzisha MyElimu, tovuti ya kisasa inayowezesha wanafunzi wa sekondari kujadiliana na kubadilisha mawazo. Tovuti hi ina nyenzo za masomo yote yanayofundishwa katika shule za sekondari nchini Tanzania. Kupitia tovuti hi mwanafunzi anaweza kujifunza nyumbani na kufaulu vizuri mitihani.

edu.jpg


Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi elfu moja wamejiunga na wanafaidika na tovuti hi. Tovuti hi ni jukwaa lilio mtandaoni la kusaidia wanafunzi katika masomo yao. Kitu kinachonistajabisha ni Given kuacha jukwaa hili kuwa huru kwa kila mwanafunzi. Kijana huyu halipishi wanafunzi kujiunga na jukwaa hili adhimu.

Mwezi uliopita Given pamoja na vijana wengine wanaofanya vitu vizuri kwa jamii kutoka nchi za jumuiya ya madola walipewa tuzo na Malkia kwa mambo wanayoyafanya katika jamii. Vile vile Given alipata nafasi ya kuzungumza na watu mbali mbali wanaofanya vizuri katika maswala ya teknolojia na uvumbuzi duniani. Lengo kubwa la Given ni kutaka kutoa mchango katika kubadilisha dunia.

11665786_1038998942792068_8262430114297995722_n.jpg

Given ni kijana shupavu na jasiri. Mbali na kufanya miradi yote hi kwa jamii, kijana huyu pia ni mwanafunzi. Vile vile ni kiongozi wa mashirika mbali mbali ya vijana.

No comments:

Post a Comment